Soma Biblia Kila Siku 1

Ibada

Kazi ya sheria imebadilika kwa ujio wa imani. Kabla ya kumwamini Yesu, tulifungwa na sheria, ikituhukumu. Hali hii ilituelekeza kwa Kristo tuliposikia habari zake njema. Na tangu tulipofika kwa Kristo, kwa imani, tumekuwa na hazina ya mambo mengi mapya na mazuri: Tulihesabiwa kuwa wenye haki kwa imani. Tumefanyika kuwa wana wa Mungu (m.26). Na tumefanywa wamoja bila ubaguzi wa jinsia, hadhi, au kinginecho chochote. Basi, tuanze Mwaka Mpya tukimvaa Kristo, tusitegemee ya mwaka uliopita.