Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 1Mfano

Soma Biblia Kila Siku 1

SIKU 29 YA 31

Bwana Yesu alifanya ishara nyingi. Kwa ishara alizozifanya alidhihirisha kwamba Ufalme wa Mungu umefika, upo na unatenda kazi. Ni ishara hizo zilizowafanya Wayahudi waliokuwa hawamwamini Yesu kupata mashaka kama kweli huyo kristo mwingine waliyemngojea ataweza kufanya ishara zaidi ya hizi alizozifanya Yesu (m.31). Je, wewe unamfuata Yesu kwa kuangalia nini? Ishara tu? Kumbuka, hata bila ishara Bwana Yesu anaweza kutufanya wana wa Mungu na warithi wa uzima wa milele tukimwamini yeye.

Andiko

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 1

Soma Biblia Kila Siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha