Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kupata Uhuru kutokana na KufadhaikaMfano

Finding Freedom From Stress

SIKU 5 YA 5

Badilisha Lengo Lako.



Mfadhaiko haustahili kufafanua historia yako. Tumejifunza mfadhaiko ni kawaida tu katika maisha, lakini Yesu anaweza kutusaidia kuushinda nguvu kupitia amani yake ya milele. Kwa hivyo, unaweza vipi salimu amri mfadhaiko na uweze kuendele mbele na maisha yako?



Lazimo tuondoe lengo letu kutoka kwa mfadhaiko na tujielekeze kwa Mungu wetu. Lakini tutaanzia wapi? Kwanza kabisa, kwamba Mungu anakujali kuhusuyotemfadhaiko wako. Iwe unaohofia kuhusu mtihani wako wa katikati ya muhula ama akili inakaribia kuruka kuhusu ni nini utakachofanya na maisha yako, Mungu wetu anajali kuhusu mambo hayo na atakupatia amani. Amani Yake sio kile unachotarajia kila mara, lakini itakua kile unachohitaji kila mara.



Kwa hivyo, chukua nafasi hii na uangalie vile unaweka kutoa malengo yako katika mfadhaiko.




  1. Abudu kabla hujawa tayari. Paula anatufunza kile tunacho hitaji kukifanya wakati kunakabiliana na mfadhaiko katika Wafilipi 4, na anafungua kwa kutueleza tufurahia ndani ya Bwana kila wakati.
    Kila wakati. Yaani, tumuabudu Mungu tunapojihisi na tusipojihisi kwa sababu hata kama hisia zetu hubadilika, Mungu habadiliki. Anastahili kuabudiwa kila wakati, hata wakati tunapitia changamoto kali. Tunapomuabudu Mungu, tunakumbuka Yeye ni nani na yale mengi aliyo tuwezesha. Na Mungu ni mkuu kuliko mfadhaiko na wasiwasi zetu.

  2. Salimisha mfadhaiko wako.Hatua yetu ya pili ni kuomba na kuachilia udhibiti. Lazima tuachilie kabisa hali zetu na tumuamini Mungu atatusaidia. Katika tafsiri ya ujumbe ya Wafilipi 4, inasema "Geuza wasiwasi wako kuwa maombi…Ni ajabu kuu kile kinachoweza kutokea Christo akikuondolea wasiwasi katika maisha yako." Kuachilia mfadhaiko inamaanisha - kujisalimisha na kutorudi nyuma.

  3. Yageuze mawazo yako. Haitosi kujaribu tuKomesha mfadhaiko. Lazima tubadili tunayo waza. Paulo anatusisitiza kufikirie yaliyo safi, sawa na yakupendeza. Yawazie haya na sio mfadhaiko wako. Kumbuka kushukuru kwa kile ulichonacho, yale Mungu aliyokubitisha na watu wanaokupenda maishani. Ruhusu shukurani hizi zijaze mayazo and moyo wako. Mwishowe, chukua mateka wazo lolote lile na ulisalimishe kwa Kristo. Badilisha "Nimefadhaika" na " Naweza yatenda yote kumpitia Kristo anayenipatia nguvu." Haribu uongo wa mfadhaiko kwa kutumia nguvu za neno la Mungu.


Unapojenga uzoefu wa kufanya vitendo hivi vitatu, utafurahia amani ya Mungu katika kila jambo. Kwa hivo, ufahamu ufadhaiko wako, chukua hatua kuibadilisha na ukweli, na uwasilishe kwa Mungu wako aliye mbinguni anayekujali. Unaweza zoea amani kila siku, kwa hivyo itafute na uache mafadhaiko nyuma.



Jadilianeni




  • Ni wazo gani katika haya mawazo matatu unastahili kuwekea mkazo kila mara?

  • Ni uongo gani mfadhaiko hukuambia kila mara? Unaweza badili uongo huu na nini?

  • Amua utakavyo tenda wakati mwengi unapojihisi unafadhaika ama umezidiwa.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Finding Freedom From Stress

Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha