Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kupata Uhuru kutokana na KufadhaikaMfano

Finding Freedom From Stress

SIKU 4 YA 5

Wacha kupatia mfadhaiko nguvu.



"Nika mfadhaiko" imekua salamu ya kawaida siku hizi, ni kama, "Niko bizi." Na tukiongea ukweli, tunaweza kutumia mfadhaiko kama chanzo cha kujivuna. Tukisema tuna mfadhaiko tunajihisi kuwa watu wa muhimu, hata kama hatuipendi hisia mfadhaiko utuletea, tunapenda hadhi inayotuletea.



Katika tamaduni yetu ya mwendo-kasi, mfadhaiko unaoneka kama kawaida. Neno mfadhaiko linapoteza maana yake mbaya na inapata uhusiano na kufanya kazi kwa bidii, kuwa na malengo na maendeleo. Tuna dhani watu waliofanikiwa ni watu wenye mfadhaiko, kwa hivyo tunakaribu zaidi. Na ukosefu wa mfadhaiko unatufanya kujiona wavivu wasio na maazimio.



Matokeo? Tunajaribu kila mara kufanya zaidi na kuwa zaidi, inayoleta-umeikisia- mfadhaiko zaidi. Tunatoa ahadi kupita kiasi kwa sababu hatuwezi sema hapana: tuna ridhika na urafiki isio kweli kwenye mitandao badala ya kuweka mda kando kuwa na gumzo zenye maana: na tunajenga mfadhaiko katika ubinafsi wetu.



Ila maisha ya mfadhaiko sio Mungu alivyo tudhania. Yesu anasema adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu. Maneno haya yanaonekana kupita kiasi, lakini mfadhaiko unaweza kuiba kutoka kwetu. Inaiba usingizi. Inaiba furaha. Inaiba uwezo wa akili zetu. Na bizi yote ile inayo weka moto mfadhaiko wetu unaweza kutu purukusha maishani hadi tunakosa mipango mikuu Mungu anayo kwetu.



Kwa mbadala, Yesu anasema Alikuja kutuletea maisha na maisha tele. Yesu alikuja kutuletea amani na tele, ambayo ni tofauti ya maisha ya mfadhailo.



Kwa hivyo ni wakati wa kutazama mfadhaiko wetu upya. Tuwache kupatia mfadhaiko mamlaka. Tuwache kutumia mfadhaiko kuringia wengine. Badala yake, tutumie kutokua na mfadhaiko kama nafasi kusimama, kuwa tofauti, na kuonyesha imani yetu.



Wakati ulimwengu unazama katika mfadhaiko, tuta chagua kuwa shwari, kimya, na kukumbuka Mungu ni Mungu. Wakati wengine wanashindana na kujilinganisha na wengine, tuta sherehekeana na kuinuana. Wakati wengine wamejawa na majonzi bila matumaini, tutakua watu ambao watabeba matumaini hadi wasio amini Mungu wata angalia na kuuliza ni kwa nini tuko ma matumaini tulio nayo.



Tunaweza kupata uhuru kutoka kwa mfadhaiko tukiwacha kuupatia nguvu na tuanze kugeuka kuelekea chanzo cha nguvu zote - Mungu wetu. Kwa hivyo tuache kuishi katika mfadhaiko na baadaye tumchukue Yesu katika Neno Lake na tuishi maisha kamili.



Tujadiliane




  • Unaweza sema ni nini chanzo kikuu cha mfadhaiko katika maisha yako?

  • Unafikiri maisha yako yangekua vipi kama ungetoa kabisa mfadhaiko?

  • Unaweza simamisha vipi kupatia nguvu mfadhaiko katika maisha yako?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Finding Freedom From Stress

Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha