Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kupata Uhuru kutokana na KufadhaikaMfano

Finding Freedom From Stress

SIKU 3 YA 5

Unaweza pata amani kamilifu



Kama umekabiliana na kufadhaika kwa mda mrefu, unatambua kwamba unaweza iairisha, upambane nayo, na uishi kuipitia, lakini huwezi izidi nguvu bila usaidizi. Mfadhaiko ni masumbuzu ya akili. Ni njia ya kupambana na mambo yanayo tufanya tujihisi tumetishiwa, tunaogopa, tuna wasiwasi, na kuangaika. Lakini hata hatuwezi kushinda mfadhaiko bila usaidizi, tuna njia ya kufikia usaidizi - amani.



Yesu anafahamika kama "Mkuu wa Amani" katika Isaya 9. Yesu alikua na ndiye ukamilisho wa amani. Yesu alipokua ulimwenguni, aliwa ahidi wanafunzi wake kwamba atawapa na kuwa achia amani yake hata atakapo rudi mbinguni. Hakuna amani mbali ya Yesu. Amani pia inafahamika kama Tunda la Roho, kwa hivyo inaeleweka kwamba ni jambo la muhimu zaida.



Kuna watu na mambo mengi ambayo yana kiri kutuletea amani katika maisha yetu: njia za kujichunga, maandiko kuhusu kutafakari, uandishi wa jarida, na machaguo mengi. Na kwa kweli kuna nafasi ya mambo haya yote katika maisha yetu, ila hamna badala ya ukweli, amani kamilifu inapatikana kwa Mungu pekee.



Katika Bibilia, moja ya maana ya kimsingi ya neno amani limetoka kutoka kwa neno la Kiwaebrania, Shalam linalo maanisha uzima. Basi haistaibishi kwamba hatuwezi pata amani bila usaidizi. Sisi ni watu tulio vunjika na hatutafuti tu suluhisho kwa mfadhaiko wetu. Kwa ukweli tunatafuta kupona kabisa. Na ni Mungu tu anayeweza kuchukua vipande vilivyo vunjika katika maisha yetu na kutuletea uzima. Hivyo ndivyo Mungu anavyo fanya na alivyo.



Na hapa kuna habari nzuri zaidi. Tuna upatikanaji wa amani ya Mungu. Isaya pia aliandika tunaweza kuwa na amani kamilifu kama akili zetu zitabaki lengo likiwa katika Mungu. Tukirudia maana ya mfadhaiko, tunagundua kwamba tunaweza kuweka uzito wetu kwa Mungu badala ya shida zetu.



Roho Mtakatifu anatusaidia kupata amani, na Yesu anatupa amani tunapo muuliza atupe amani. Kwa hivyo leo, jua kwamba uwezi miliki mfadhaiko bila msaada, lakini unaweza mtafuta Yule anaye weza. Na unaweza pata uponyaji wa undani zaidi katika harakati hiyo.



Mjadala




  • Ni njia gani umejaribu kutafuta amani bila usaidizi?

  • Unaweza anza vipi kutafuta amani ya kweli?

  • Ni mwahali gani ambako kumevunjika katika maisha yako kunako hitaji uponyaji na uzima?
siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Finding Freedom From Stress

Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha