Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kupata Uhuru kutokana na KufadhaikaMfano

Finding Freedom From Stress

SIKU 2 YA 5

Je, unawekelea mkazo jambo gani?



Maana moja ya kwanza ya neno "Mfadhaiko" ni "usiku mkesha" ambayo ni maana ya karibu sana kulinganisha vile mfadhaiko unahisi. Unahisi kana kwamba uwezi pumua ama kufikiria - ni kama umebanwa. Miaka michache baadaye, neno mfadhaiko limepata maana ya mfano tofauti. Maana ya mbeleni kabisa ilikua "kuweka mkazo" ama "kusisitiza kwa kuwekelea uzito."



Tena, imepiga msumari kichwani, kweli? Tunapo fadhaika kuhusu jambo fulani, tuna wekelea mkazo shida zetu. Na saa zingine hivyo ni sawa, lakini lazima tujiulize- je tunawekelea uzito shida zetu ama Mungu?



Yesu alitupa changamoto kuhusu swala hili katika Mathayo 6. Anafafanua kwamba hatuhitaji kuhangaika kuhusu ni jambo gani litakalo tokea tena katika maisha yetu. Badala yake, Anatualika kumuamini. Anatuimarisha tuzingatie kama kweli Yeye ni Mungu mwema anayetujali kwa sababu kama tunaamini kwa kweli anatutakia mema, basi tunaweza kuacha kuzingatia sana ni nini kiko mbele yetu.



Jambo moja kuu ambalo Yesu alisema ni, "Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa." Mathayo 6:33 SNT)



Yesu anafahamu vyema kutuliko tunachohitaji duniani. Lakini tunajaribu kuishi maisha mema na kusahau kutilia mkazo maisha ya milele. Tunajua ulimwengu huu si nyumbani mwetu. Lakini tunaabudu starehe. Kinacho tufadhaisha zaidi hounesha tunacho kijali maishani. Na kama kila mara tunajali kupata makuu humu duniani, tunafaa kujiuliza kama maisha mioyoni mwetu yana lingana na ufalme wa Mungu ama tunalenga kujenga ufalme wetu wenyewe.



Ata kama tunastahili kutumia vipaji vyetu kufanya tofauti katika ulimwengu huu, hakuna ubaya na kuwa na matarajio, ila tuhakikishe malengo yetu makuu ni ufalme wa Mungu. Utafute kwanza Ufalme wa Mungu- na mengine utaongezewa.



Kwa hiyo, unavyo tafakari kuhusu mfadhaiko, jiulize unategemea nini. Unatilia mkazo nini?



Chagua kwanza kumtegemea Mungu. Chagua kumuamini kwamba ni Baba mwema ambaye anakujali. Na unapo mwangazia Mungu na sio wewe binafsi, utashanga jinsi kufadhaika kwako kutakua kitu kidogo sana.



Mjadala




  • Ukiwa mkweli, ni nini ambacho umekua ukisisitiza sana hivi karibuni?

  • Je ni njia gani unaweza kuanza kuelekeza lengo lako kwa Mungu na mbali na mfadhaiko?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Finding Freedom From Stress

Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha