Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: MosaicMfano

Devotions for Lent from Holy Bible: Mosaic

SIKU 8 YA 46

Sadaka yenye Shimo (Eileen Button)

Kama watoto wengine wengi wa kikatoliki, nilitoa peremende kwa siku zaidi ya arobaini za Kwaresima. Nakumbuka nikiteremka chini polepole asubuhi ya Pasaka, nikitarajia kupata chokoleti tamu ya Palmer's. Baada ya kumaliza msimu mgumu wa sadaka, singeweza ngojea kukula hiyo chokoleti.

Ningesikitika sana kupata chokoleti yenye shimo katika kikapu changu badala ya chokoleti niliyopenda. Walakini kulikuwa na chokoleti ya maziwa ikiwa imechukuwa muundo wa msalaba. Kitu kilichotumika kumtesa Mkombozi wangu. Badala ya mwili wa Kristo, kulikuwa na maua ya rangi ya waridi na njano iliyotengenezwa kwa sukari. Singeweza kula. Ilikuwa kama kufuru kufanya hivyo. Wakati ilikuwa vigumu sana kumaliza siku za Kwaresima bila vitu vitamu, sadaka yangu isiyo ya maana ilinishtua nilipokutana na chokoleti hiyo asubuhi ya Pasaka. Hata mtoto hushangazwa na sadaka ambayo Kristo alitoa ya maisha yake.

Msimu wa kila mwaka wa Kwaresima ni fumbo ngumu kwa wengi. Kujinyima vitu tunavyovipenda au tabia tunazopenda - hata kwa muda kidogo - inaonekana kama kitu kilichopitwa na wakati katika tamaduni yetu ya "naitaka sasa hivi". Kwaresima ni muda usiotamanika unaotuelekeza katika kelele mbaya za Ijumaa Kuu na Jumapili ya Pasaka nzuri. Ni msimu wa kusudi na nia..

Walakini huwa tuna sahau nia na kusudio la msimu huu. Tunapofunga na kujinyima chochote kile kinachochukua nafasi ya Mungu, tunawezajaribiwa tukawa na kiburi kuhusu sadaka yetu. Kile ambacho tunajinyima kinaweza kujitokeza ndani mwetu kama haja ya kutimizwa. Badala ya kuweka lengo letu kwa Mungu, tunaweza tukajipata tunalenga kile ambacho tumejinyima.

Hata hivyo, zoezi la Kwaresima linaweza kuwa nidhamu ya manufaa. Ni vigumu kutambua ni nini hisia zetu daima za haki zetu zinafanyia miili yetu na nafsi. Tamaduni zetu huabudu raha za dunia na kuinamia vitu vitamu tunavyopewa. Na tukiendelea hivyo tunaweza tukakosa ufahamu wa mahitaji yetu - njaa ya ukweli - maishani mwetu. Tukifwata Kwaresima tunaweza tukaelewa na kupigana na matumizi yetu. Tukiamua kuachana na kile ambacho hakitutoshelezi kikamilifu, tunapatana uso kwa uso ka maswali magumu. Tunaweza kuamini Yesu anaposema, "Watu hawataishi kwa mkate peke bali kwa neno linalotoka kinywani mwa Mungu"? Tunawezaje tengeneza sehemu ya Mkombozi katika maisha yetu ya dhiki? Tunaweza tukaelewa ukweli ya Ijumaa Kuu na tuishi na kejeli lake?

Kwaresima inatupa changamoto ya kutafuta majibu aminifu ya maswali haya na mengine mengi ya kutafuta nafsi. Inatualika tuachane na maisha ya matumizi na tamaa ya kila siku. Ina uwezo wa kutupatia pumziko tunalohitaji kutokana na tamaa na mahitaji yasiyofaa.

Kama waumini wengine, ninashikilia sana nidhamu ya Kwaresima na nitaendelea kuacha kitu ambacho ninatumia. Nina enzi sana msimu wa kujinyima, kutafuta na ufunuo. Kila mwaka ninajifunza kitu kipya.

Labda bado nakerwa na chokoleti yenye shimo kwa sababu inaonyesha ukweli wa maisha yetu ya kiroho: tunachokiona nje kinaweza kikawa kizuri lakini tunaweza tukawa tupu kabisa. Mara kwa mara, ukweli wa sadaka ya Kristo na nguvu za upendo wake huingia ndani ya mioyo yetu migumu. Utambuzi huu, kama maji baridi yaliyoganda kwa nyuso zetu, zilizochoka hutufanya kushtuka. Shimo katika shemu ya nafsi zetu zinaweza kujazwa.

Kuhusu Mpango huu

Devotions for Lent from Holy Bible: Mosaic

Ibada Hii ya kila siku kwa siku 46 kabla ya Pasaka iliyochukuliwa kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic, inaleta pamoja dondoo, masomo na maandiko kukusaidia kulenga akili yako kwa Kristo. Ikiwa huna uhakika msimu wa kabla ya Pasaka unahusu nini au umekuwa ukijihusisha na msimu huu maisha yako yote, utafurahia masomo ya maandiko na ibada za busara kutoka kwa Wakristo kote ulimwenguni na katika historia. Jiunge nasi na kanisa kote duniani kulenga akili zetu kwake Yesu katika wiki zote za kabla ya Pasaka.

More

Tungependa kushukuru Wachapishaji wa Tyndale House kwa ukarimu wao wa kutoa Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic Kujifundisha mengi kuhusu Biblia Takatifu: Mosaic tafadhali tembelea: www.tyndale.com/p/holy-bible-mosaic-nlt/9781414322056