Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: MosaicMfano

Msimu Kabla ya Pasaka ni nini?
Kwa Wakristo wengine, Msimu kabla ya Pasaka umekuwa sehemu ya maisha yao ya kiroho, lakini kwa wengine hawana habari. Huu ni msimu unaotuelekeza kwa Pasaka, wakati ambao Wakristo kihistoria wametayarisha mioyo yao kwa Pasaka kwa kutafakari, kutubu na maombi. Msimu Kabla ya Pasaka huanza na Jumatano ya Ashi na huendelea kwa siku arobaini, bila kujumuisha Jumapili, na huishia na Ijumaa Kuu na Jumamosi Takatifu. Kwa sababu Jumapili ni sherehe za kufufuka kwa Yesu kila wiki, Jumapili sita za kabla ya Pasaka hazihesabiwi kama sehemu ya msimu huu wa siku arobaini, ambao hulenga kujichunguza, kujiangalia na kutubu. Wakristo wengi huchagua kusherehekea kufunga msimu wote wa kabla ya Pasaka, Lakini lengo sio kujinyima kitu bali kujishughulisha na Mungu na nia yake duniani
Msimu kabla ya Pasaka ni msimu muhimu sana katika mwaka wa kanisa. Mwaka wa kanisa ni njia bora ya kutusaidia kumpa Mungu kipaumbele katika mipango yetu. Badala ya kufuata muundo unaojulikana wa kalenda ya nishati ya jua, uliopangwa kwa mipangilio asilia, kalenda ya kanisa imepangwa kujihusisha na Mungu na matendo yake duniani. Kalenda ya kanisa hufuata misimu sita tofauti: Ujio, Krismasi, Epifania, Kabla ya Pasaka, Pasaka na Pentekoste. Misimu hii ina malengo tofauti: Ujio unalenga ujio wa Mungu duniani, kimwili na kurudi kwake Kristo. Krismasi inalenga kuzaliwa kwake Kristo. Epifania inalenga nuru ya uwepo wa Mungu ukiangaza duniani. Kabla ya Pasaka hulenga dhambi za binadamu na suluhu yake Mungu. Pasaka hulenga ufufuo wa maisha. Pentekoste hulenga matendo yanayoendelea ya Roho Mtakatifu duniani. Mipangilio ya kila mwaka ya misimu hii inaweza kuwa na athari zenye nguvu katika ukuaji wa kiroho wa mtu binafsi au jumuia.
Ikiwa umefurahia ibada hii ya Msimu kabla ya Pasaka, basi angalia Biblia Takatifu: Mosaic, Biblia ilyochapishwa inayojumuisha kila kitu ulichokisoma katika ibada hii, michoro yenye rangi na masomo ya mwaka wa kanisa ya kila wiki.

Andiko
Kuhusu Mpango huu

Ibada Hii ya kila siku kwa siku 46 kabla ya Pasaka iliyochukuliwa kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic, inaleta pamoja dondoo, masomo na maandiko kukusaidia kulenga akili yako kwa Kristo. Ikiwa huna uhakika msimu wa kabla ya Pasaka unahusu nini au umekuwa ukijihusisha na msimu huu maisha yako yote, utafurahia masomo ya maandiko na ibada za busara kutoka kwa Wakristo kote ulimwenguni na katika historia. Jiunge nasi na kanisa kote duniani kulenga akili zetu kwake Yesu katika wiki zote za kabla ya Pasaka.
More
Tungependa kushukuru Wachapishaji wa Tyndale House kwa ukarimu wao wa kutoa Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic Kujifundisha mengi kuhusu Biblia Takatifu: Mosaic tafadhali tembelea: www.tyndale.com/p/holy-bible-mosaic-nlt/9781414322056