Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: MosaicMfano

Devotions for Lent from Holy Bible: Mosaic

SIKU 6 YA 46

Kutambua Kutoridhika

Msimu wa Kwaresima hutuonyesha huzuni ya Yesu siku za mwisho kabla ya kusulubiwa. Tunaposoma maongezi binafsi ya Yesu na wanafunzi wake katika chumba cha juu, tunafikiria furaha ya urafiki pamoja na huzuni ya usaliti wa rafiki. Tunapoingia katika giza la kukamatwa kwa Yesu, kesi na kuchapwa, tunalia na wale Wakristo wa kwanza, na katika juhudi zetu za kuokoa Yesu kutoka kwetu sisi wenyewe, tunahuzunika kama usaliti wa Petro. Desturi ya Kwaresima - sadaka ya siku arobaini - ni njia moja ya kuomboleza kifo kilichosababishwa na dhambi katika maisha yetu. Tunapoona Yesu akistahimili kikamilifu majaribio ya shetani jangwani, tunakubali dosari zetu, sadaka zetu duni. Wakati huu wa kukata tamaa una njia ya kushangaza ya kutukumbusha haja tulionayo na Yesu Kristo.

Kuhusu Mpango huu

Devotions for Lent from Holy Bible: Mosaic

Ibada Hii ya kila siku kwa siku 46 kabla ya Pasaka iliyochukuliwa kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic, inaleta pamoja dondoo, masomo na maandiko kukusaidia kulenga akili yako kwa Kristo. Ikiwa huna uhakika msimu wa kabla ya Pasaka unahusu nini au umekuwa ukijihusisha na msimu huu maisha yako yote, utafurahia masomo ya maandiko na ibada za busara kutoka kwa Wakristo kote ulimwenguni na katika historia. Jiunge nasi na kanisa kote duniani kulenga akili zetu kwake Yesu katika wiki zote za kabla ya Pasaka.

More

Tungependa kushukuru Wachapishaji wa Tyndale House kwa ukarimu wao wa kutoa Ibada za kabla ya Pasaka kutoka kwa Biblia Takatifu: Mosaic Kujifundisha mengi kuhusu Biblia Takatifu: Mosaic tafadhali tembelea: www.tyndale.com/p/holy-bible-mosaic-nlt/9781414322056