Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Neno la Mungu Kwa Kila HitajiMfano

God's Word For Every Need

SIKU 5 YA 5

MAPENZI YANAYOONEKANA

“Baba anakupenda.”

Usiku ule kabla hajafariki, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba Baba anawapenda. Neno "upendo" hapa halioneshi wajibu au kujisahau, dhabihu ya kujitoa. Linabeba hali ya "kuonesha mapenzi" --upendo uliojaa joto na umeoneshwa waziwazi. Hili ni muhimu sana kulielewa. Upendo wa Baba si wajibu au upendo wa kawaida. Hapana, maana ya maneno ya Yesu hapa ni kwamba "Baba anakupenda sana, kwa dhati na kuonekana." Ni upendo mkubwa kiasi gani huu! Wababa wengi wa duniani wako mbali, kimwili au kihisia. Hivi sivyo kwa Baba yetu wa mbinguni; Yesu alipokufa na kufufuka tena, alipaa kwenda mbinguni na huko alimimina Roho Mtakatifu kwa waamini wake. Aliwajaza wanafunzi wake na Roho ya kuasili na walianza kuita "Baba!" Kuanzia wakati huo na kuendelea, walijua Baba aliwapenda kwa mapenzi yaliyooneshwa --kwa mikono yake yenye nguvu na kufariji kwa upendo. Hivi ndivyo Yesu anatutaka na sisi pia. Hebu tumuombe atusaidie kutambua hilo mioyoni mwetu, na siyo vichwani mwetu. Hebu tupate mapenzi ya Baba yaliyooneshwa.

OMBI

Bwana Yesu, ninakuomba unisaidie kujua moyoni mwangu kwamba Baba mwenyewe ananipenda sana, kwa moyo wote na kwa kudhihirisha. Katika jina lako. Amen.

Jifunze zaidi katika Destiny Image Publishers, au jifunze zaidi kupitia kitabu katika Amazon or Barnes and Noble.

Andiko

Kuhusu Mpango huu

God's Word For Every Need

Maisha yanaweza kuwa magumu, na unapokabiliwa na changamoto na unahitaji kutiwa moyo, mahali bora pa kwenda ni kwenye neno la Mungu. Lakini wakati mwingine ni vigumu kujua uangalie wapi. Neno la Mungu kwa Kila Hitaji linajumuisha maandiko muhimu kwa kila mwanafunzi wa Neno kutafuta wakati kupanda na kushuka katika maisha. Mtegemee Mungu kukusaidia katika nyakati ngumu.

More

Tungependa kuwashukuru wachapishaji wa Destiny Image kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.destinyimage.com