Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Neno la Mungu Kwa Kila HitajiMfano

God's Word For Every Need

SIKU 2 YA 5

UTAMBULISHO WETU HALISI

“Mtakuwa wana na mabinti kwangu.”

Kila baba mwema ana ndoto kwa ajili ya watoto wake. Katika mafundisho yaliyopita tuliona sehemu ya ndoto ya Mungu kwetu: “Nitakuwa Baba kwenu.” Huo umekuwa mpango wake hata kabla ya kuumbwa kwa misingi ya dunia. Lakini kuna zaidi. Siyo tuu Mungu anataka tujue utambulisho wake halisi; anataka pia tujue utambulisho wetu halisi. Kama yeye ni baba yetu, kwa hiyo sisi ni nani? Kama tukichagua kumfuata mwanaye, Yesu Kristo, inatufanya kuwa wana na mabinti zake. Hii ni furaha kubwa sana --kujua kwamba Mungu ni baba tuliyekuwa tunamngoja, na kufurahia upendeleo wa kuwa wana na mabinti wa Baba mkuu kuliko wote. Hii ni ndoto yake kwa maisha yetu. Hebu tufanye hili kuwa lengo letu kuu kuingia katika utimilifu wa maana ya kuwa wana na mabinti wa Baba mkuu kuliko wote. Hebu tufanye kuwa ni lengo la maisha yetu kuwa watoto bora wa Baba yetu wa mbinguni. Hii ni ndoto ya Baba kwa maisha yetu. Na tuifanye kuwa ndoto yetu pia.

OMBI

Baba yetu, ninakushukuru kwamba umeniita kuwa mwana wako wa kuasili. Nisaidie kujenga utambulisho wangu kwa heshima hii ya ajabu. Katika jina la Yesu. Amen.

Andiko

Kuhusu Mpango huu

God's Word For Every Need

Maisha yanaweza kuwa magumu, na unapokabiliwa na changamoto na unahitaji kutiwa moyo, mahali bora pa kwenda ni kwenye neno la Mungu. Lakini wakati mwingine ni vigumu kujua uangalie wapi. Neno la Mungu kwa Kila Hitaji linajumuisha maandiko muhimu kwa kila mwanafunzi wa Neno kutafuta wakati kupanda na kushuka katika maisha. Mtegemee Mungu kukusaidia katika nyakati ngumu.

More

Tungependa kuwashukuru wachapishaji wa Destiny Image kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.destinyimage.com