Neno la Mungu Kwa Kila HitajiMfano

UPENDO WA UPENDO WOTE
Ni upendo wa ajabu kiasi gani Baba aliotupa!
Hakuna furaha kubwa duniani zaidi ya kujua kwamba Mungu ni Baba anayetupenda, bado watu wengi, ikijumuisha walio kanisani, hawajapata furaha hii isiyosemekana. Wengi wamejeruhiwa na baba zao wa duniani na, matokeo yake, wanauangalia ubaba huo katika Mungu Baba. Wanamuangalia Mungu katika taswira ya baba zao wa duniani --wakimwangalia kama baba asiyekuwepo au baba anayetelekeza. Wengine wanamuangalia kama baba aliye mbali na baba mwenye kisasi. Hakuna katika taswira hizo ni kiwakilishi halisi cha taswira Yesu anayoichora. Yesu alikuja kuufunua upendo wa ajabu wa Baba. Ndiyo Mungu ni Mfalme. Ndiyo Mungu ni Bwana. Ndiyo Mungu ni Hakimu. Lakini amekuwa daima ni Baba aliyependa sana ulimwengu huu yatima mpaka akamtuma mwana wake wa pekee kuwafanya watumwa kuwa wana na yatima kuwa warithi. Hii ni baraka kubwa sana --kujua kwamba Mungu ni Baba mkuu. Kama ulimkosa baba mzuri hapa duniani, jua hili: Una Baba mkamilifu Mbinguni na ametoa upendo wake wa ajabu kwako katika Yesu.
OMBI
Baba, ninakushukuru kwamba hauko mbali bali karibu. Nisaidie kufurahia ukaribu na wewe ninaposoma mafundisho haya. Katika jina la Yesu. Amen.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Maisha yanaweza kuwa magumu, na unapokabiliwa na changamoto na unahitaji kutiwa moyo, mahali bora pa kwenda ni kwenye neno la Mungu. Lakini wakati mwingine ni vigumu kujua uangalie wapi. Neno la Mungu kwa Kila Hitaji linajumuisha maandiko muhimu kwa kila mwanafunzi wa Neno kutafuta wakati kupanda na kushuka katika maisha. Mtegemee Mungu kukusaidia katika nyakati ngumu.
More