Neno la Mungu Kwa Kila HitajiMfano

MWALIKO WA KIMBINGU
“Nitakuwa Baba kwenu.”
Ni mstari gani muhimu katika Biblia? Watu wengi watasema, “Yohana 3:16: Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee.” Hata hivyo, mstari huu kutoka waraka wa pili wa Paulo kwa Wakorintho unaweza kuleta tofauti kubwa pia. Kwa namna, mpango mzima na kusudi la Mungu vinaweza kuelezwa kwa kifupi kwenye maneno, "nitakuwa Baba kwenu." Huu umekuwa ni mpango wa Mungu tangu Adamu na Hawa walipotenda dhambi katika Bustani ya Edeni. Ilipotokea hivyo, wanadamu walitenganishwa na upendo wa Baba. Matokeo yake, tulikuwa yatima wa kiroho --hatukuhusika tena na Mungu kama Baba yetu. Lakini ashukuriwe Yesu, yote hayo yamebadilika! Yesu ni jibu katika hali yetu ya kuwa yatima. Alikuja hapa ulimwenguni kufa kwa ajili ya dhambi zetu na kutuasili kwenye familia ya Baba hapa duniani. Sasa tunaweza kumwita Mungu "Baba" na kutulia kwenye mikono yake ya upendo. Katika kitabu hiki cha ibada, Yesu anatualika kuitikia maneno haya ya wakati wote: "Nitakuwa Baba kwenu."
OMBI
Asante, Mungu, kwa mwaliko wako kukujua kama Baba. Kwa moyo wangu wote nasema "Ndiyo," napoanza mfululizo huu wa masomo. Katika jina la Yesu. Amen.
Jifunze zaidi katika Destiny Image Publishers, au jifunze zaidi kuhusu kitabu kupitia Amazon or Barnes and Noble.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Maisha yanaweza kuwa magumu, na unapokabiliwa na changamoto na unahitaji kutiwa moyo, mahali bora pa kwenda ni kwenye neno la Mungu. Lakini wakati mwingine ni vigumu kujua uangalie wapi. Neno la Mungu kwa Kila Hitaji linajumuisha maandiko muhimu kwa kila mwanafunzi wa Neno kutafuta wakati kupanda na kushuka katika maisha. Mtegemee Mungu kukusaidia katika nyakati ngumu.
More