Neno la Mungu Kwa Kila HitajiMfano

WANA WA MUNGU
Hebu angalia—tunaitwa wana wa Mungu!
Katika masomo yaliyopita tuliona kwamba Mungu ni Baba ambaye ameonesha upendo wake wa ajabu kwetu. Moja kwa moja baada ya kusisitiza hili, Mtume Yohana anatukumbusha kwamba, kama tumechagua kumfuata Yesu, tunaitwa "wana wa Mungu." Hivi ndivyo hakika tulivyo. Huu ndiyo utambulisho wetu halisi. Taswira yetu haitegemei tunafanya nini. Thamani yetu haitegemei mafanikio yetu. Hapana, utambulisho wetu halisi umejengwa kwenye kitu cha kudumu zaidi na salama. Ni msingi gani mzuri zaidi ya ufunuo wa Agano Jipya --kwamba wote wanaomjua Yesu ni wana na mabinti walioasiliwa wa Baba? Ndivyo unavyojiona? Kama sivyo, naomba nikuhimize kujenga utambulisho wako katika ukweli huu. Nikutie moyo kufanya kile ambacho Mtume Yohana anasema hapa na "hebu tazama." Fikiria, tafakari, waza ukweli huu na ufurahie uzuri wake. Ukifanya hivyo, siku zote utakuwa na uhakika kwamba usalama wako uko kwenye nafasi yako kama mwana wa Mungu, na siyo kwa matendo yako.
OMBI
Mpendwa Baba, napenda kukupa sifa kwamba unanipenda kwa jinsi nilivyo --mwana wa Mungu. Asante kwa heshima hii. Katika jina la Yesu. Amen.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Maisha yanaweza kuwa magumu, na unapokabiliwa na changamoto na unahitaji kutiwa moyo, mahali bora pa kwenda ni kwenye neno la Mungu. Lakini wakati mwingine ni vigumu kujua uangalie wapi. Neno la Mungu kwa Kila Hitaji linajumuisha maandiko muhimu kwa kila mwanafunzi wa Neno kutafuta wakati kupanda na kushuka katika maisha. Mtegemee Mungu kukusaidia katika nyakati ngumu.
More