1
Waefeso 6:12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Mapigano yetu si juu ya watu duniani. Tunapigana dhidi ya watawala, mamlaka na nguvu za giza za ulimwengu huu. Tunapigana dhidi ya nguvu za uovu katika ulimwengu wa roho.
Linganisha
Chunguza Waefeso 6:12
2
Waefeso 6:18
Ombeni katika Roho kila wakati. Ombeni maombi ya aina zote, na ombeni kila mnachohitaji. Ili mfanye hivi ni lazima muwe tayari. Msikate tamaa. Waombeeni watu wa Mungu daima.
Chunguza Waefeso 6:18
3
Waefeso 6:11
Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kupigana dhidi ya hila za Shetani.
Chunguza Waefeso 6:11
4
Waefeso 6:13
Ndiyo sababu mnahitaji silaha zote za Mungu. Ili siku ya uovu, mweze kusimama imara. Na mtakapomaliza mapigano yote, mtaendelea kusimama.
Chunguza Waefeso 6:13
5
Waefeso 6:16-17
Pia itumieni ngao ya imani ambayo itatumika kuizuia mishale inayowaka moto inayotoka kwa yule Mwovu. Upokeeni wokovu wa Mungu kama chapeo yenu. Na chukueni upanga wa Roho, yaani mafundisho ya Mungu.
Chunguza Waefeso 6:16-17
6
Waefeso 6:14-15
Hivyo simameni imara mkiwa mmefungwa mkanda wa kweli viunoni mwenu, na katika vifua vyenu mkiwa mmevaa kinga ya maisha ya haki. Miguuni mwenu vaeni Habari Njema za amani ili ziwasaidie msimame imara.
Chunguza Waefeso 6:14-15
7
Waefeso 6:10
Hapa lipo neno moja la mwisho la ushauri: Mtegemeeni Bwana kwa ajili ya nguvu zenu. Wekeni matumaini yenu katika nguvu zake kuu.
Chunguza Waefeso 6:10
8
Waefeso 6:2-3
Amri husema, “Waheshimu baba yako na mama yako.” Hii ndiyo amri ya kwanza iliyo na ahadi pamoja nayo. Na hii ndiyo ahadi: “Ndipo utakapofanikiwa, na utakuwa na maisha marefu duniani.”
Chunguza Waefeso 6:2-3
9
Waefeso 6:1
Watoto, watiini wazazi wenu katika namna ambayo Bwana anataka, kwa sababu hili ni jambo sahihi kutenda.
Chunguza Waefeso 6:1
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video