YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

DAY 7 OF 31

Dhabihu zilizotolewa katika Agano la Kale hazikuweza kuondoa dhambi. Hata zililetakumbukumbuyake kila mwaka, zikitolewa kwa ajili ya dhambi zilezile. Hivyo watoaji walijifunza kutazamia dhabihu ile ambapo Yesu alikuja kuitoa. Kujitoa kwake msalabani kuna ubora wa kuondoa kumbukumbu ya dhambi. Tunapopata msamaha tuamini kuwa hata kumbukumbu ya dhambi zetu imefutwa mbele za Mungu. Ndivyo Mungu mwenyewe alivyoahidi:Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa(Ebr 10:17). Hivyo tunayo amani na Mungu. Hii itatusaidia kuleta amani hata katika mahusiano yetu na watu wengine.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More