Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Sample

Mfano wa viti vya mbele una maana gani? Yesu alipotoa mifano alitaka kutufundisha mambo muhimu kuhusu Ufalme wa Mungu. Kwa hiyo mfano huu hauhusu tu unyenyekevu katika maisha haya, ila zaidi unahusu namna ya kupata kuingia karamuni Mbinguni. Hapo panatakiwa unyenyekevu. Ndivyo anavyosema Yakobo, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu (Yak 4:6). Kumbuka pia ilivyoandikwa katika Mt 18:1-4, Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema, Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Na unakumbushwa kuwa ... ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri (m.13). Mungu hututendea mema mengi bila kudai malipo. Anatuita tutende vivyo hivyo! Je, umefuata agizo hili maishani mwako?
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Related Plans

FruitFULL - Faithfulness, Gentleness, and Self-Control - the Mature Expression of Faith

Peace in Chaos for Families: 3 Days to Resilient Faith

Daniel in the Lions’ Den – 3-Day Devotional for Families

The Bible, Simplified

Spring of Renewal

Connect

Rich Dad, Poor Son

What Is My Calling?

Beautifully Blended | Devotions for Couples
