YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Upendo Wa BureSample

Upendo Wa Bure

DAY 4 OF 5

Kutoka Maisha ya changamoto na shida hadi Maisha ya Unyonge Watu wanaolisha au kuwachunga nguruwe wanaanza kuiga tabia za nguruwe. Njaa iliyomkumba Mwana Mpotevu ilimlazimisha kula chakula kibofu sana lakini, hakunawiri au kushibishwa na chakula hiki. Alianza maisha yake akiwa anafuata anasa, mafanikio, mapenzi na raha lakini alipata vitalu au vizuizi kote alikoenda. Baada ya kutapanya mali yake yote, alijipata kuwa mnyonge na bado, hakutosheka katika maisha yake. Mithali 15:21 inatueleza hivi, “Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu huunyosha mwenendo wake.” Upungufu wa Mwana Mpotevu ulisababisha raha za wakati mfupi, lakini, alihitaji ujuzi mufti na ukosefu wa ujuzi huu ulimwacha katika shida kubwa, shida ambazo hakutegemea kupata. Ninakutana na watu wengi sana walio katika vyumba au makao ya nguruwe, watu ‘wanaokula’ vyakula vibofu kabisa wakijaribu kutosheleza upweke ulio katika mioyo yao. Ilhali, haijalishi jinsi wanavyojaribu, bado wanabakia wakiwa wapweke, katika hali ya kutoridhika na mioyo yenye machungu kama shimo la giza - roho tupu zinazohitaji kujazwa….na hakuna anayeweza kuwapa riziki inayoleta mabadilko. Watu wengi wanacheza karata ya kadi katika maisha yao, matokeo yakiwa mahusiano, mafanikio ya kifedha, umaarufu katika jumuiya au kuheshimika au kupata mamlaka katika mambo ya kidini na kuzoroteka hadi kujiunga na tabia za ngono, kutumia madawa za kulevya na burudani zisiofaa. Haijalishi wanapojipata maishani, yaani, wakiwa upande wa hekima au maisha ya uharibifu, inakuwa wazi kwamba roho unaoishi milele hauwezi kunusurishwa na mambo ya kidunia. Basi, safari ya Mwana Mpotevu likuwa ya mviringo katika mauti iliyo vigumu sana kuepuka mpaka wakati alirudisha fahamu na kuwaza, “Mambo haya yalifanyika vipi? Nilifikia hapa vipi? Kunaye atakaye nisaidia? Au, nitateketea katika changamoto zangu?”
Day 3Day 5

About this Plan

Upendo Wa Bure

Kunayo kusudi au sababu la maana sana katika maisha yako inayopita fikira au mawazo yako. Unaifahamu. Unahisi jambo hili moyoni mwako. Kijitabu hiki kitakuwa nguzo ya kubadilisha maisha ya wote watakayo kisoma. Funzo au ...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy