YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Upendo Wa BureSample

Upendo Wa Bure

DAY 3 OF 5

Kutoka Kuishi Hovyo hadi Maisha Duni Mali au urithi aliopata kutoka Baba yake ilizoroteka kwa haraka na kusababisha bahati mbaya iliyomletea uharibifu kamili ya kifedha. Wakati pesa zaske zilipoisha kabisa, marafiki wake pia walitoweka. Isitoshe, janga kuu likaanza akawa yuko mpweke kabisa! Watu wengi walikuwa na njaa ikawa hakuna angeweza kumsaidia - hangeweza hata kujisaidia mwenyewe. Luka 15:14-16 inaeleza jinsi alivyongangana kupata riziki. “Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote naye akawa hana cho chote. 15 Kwa hiyo akaomba kibarua kwa raia mmoja wa nchi hiyo aliyemtuma shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akatamani kujishibisha kwa maganda waliyokuwa wanakula nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa cho chote cha kula.” Mstari wa 14 unasema kwamba alikuwa “katika shida.” Tazama kwa muda, mitindo yake ya ubinafsi yalimwacha Mwana Mpotevu bila uwezo wa kupata usaidizi. Alikuwa hana chochote na mwenye shida. Kinachoshangaza kweli ni jinsi alivyotapanya pesa zake zote akijivinjari na kwa matumizi ya kimwili badala ya kutosheka na kuhifadhi urithi wake, alibaki akiwa mpweke kuliko mbeleni. Kilele cha shida zake kilikuwa wakati aliajiriwa kufanya kazi ya chini kabisa - kulisha nguruwe na kuishi nao. Haya ni matokeo ya hakika “kuishi maisha ya hovyo na anasa” na mwelekezo wa kweli katika maisha haya duni. Furaha inadumu kwa muda, wakati njaa za maisha zinapotokea, unakuwa mtu mwenye masikitiko, mwenye kinyongo na kisasi, ambaye hana faida kwako binafsi au kwa mtu mwingine yeyote. Badala ya kuwa mtu anayejihusisha na kazi ya punguza shida na changamoto duniani, unakuwa mojawapo wa changamoto zilizoko. Basi, alikuwa pale, akiishi na nguruwe na mtazamo au fikra za kujilaumu kuhusu safari yake kutoka maisha upendo wa dhati hadi maisha ya anasa mpaka maisha ya unyonge.

Scripture

Day 2Day 4

About this Plan

Upendo Wa Bure

Kunayo kusudi au sababu la maana sana katika maisha yako inayopita fikira au mawazo yako. Unaifahamu. Unahisi jambo hili moyoni mwako. Kijitabu hiki kitakuwa nguzo ya kubadilisha maisha ya wote watakayo kisoma. Funzo au ...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy