YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Upendo Wa BureSample

Upendo Wa Bure

DAY 1 OF 5

Neno ambalo linalomueleza Mungu zaidi kuliko maneno yote Wakati Yesu aliwahimiza wafuasi wake kutegemea Mungu kutimiza matakwa au mahitaji yao, alionyesha mifano ya uaminifu wa Mungu unao onyeshwa wazi katika mazingira yao. Aliendelea kueleza jinsi Mungu aliwalisha ndege au Kunguru na kurembesha ardhi na maua maridadi akiwahakikishia wafuasi wake jinsi walivyo na thamani kuliko ndege na maua au mimea kwa jumla. Alipomaliza kuwahimiza kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza, na kuamini kikamilifu kuhusu mambo yengine yote, limalizia kwa kusema, “Ninyi kundi dogo, msiogope kwa maana Mungu amependa mtawale naye katika ufalme wake.” (Luka 12:32). Yesu alifahamu jinsi watu wanavyokosa usalama au kutoamini swala la kutegemea Mungu asiyeonekana. Huyu Mungu amepitia hisia zetu tano, Ilhali, ni nguvu zake zinatuwezesha kuwa na hisia hizi. Yesu alifahamu ya kwamba itabidi kuwa na imani ya ujasiri kuamini upendo uliotolewa ovyo na Mwenyezi Mungu. Basi, alisawazisha kiini na ubinafsi wa Mungu kuwa kama Baba yao. Aliwatia moyo na kuziinua roho zao kwa kuwaeleza ilikuwa upendo wa Mungu kuwapa wana wake urithi wa Uflame wake. Ndivyo, aliwajulisha kwamba anawapenda sana na atawashughulikia watoto wake. Katika vitabu vyote vya injili, neno ambalo Yesu alitumia sana kuelezea asili ya Mungu ni neno “Baba.” Katika lugha ya kiasili au lugha ya mbeleni, jina la “Baba” linatumiwa kwa mtu ambaye ako na upendo mwingi - leo, linatafsiriwa kuwa “Daddy.” Kama kunaye mtu ambaye anaweza kukupenda bure, yaani, akupende kuliko binadamu yeyote, ni Baba yako - na jambo hili ndilo Yesu alitaka wafuasi waelewe kikamilifu kuhusu Mungu. Alitaka wajue kwamba Mungu ni Baba yao na amejitolea kuwapenda sana, kuwapenda bure bila kujali.
Day 2

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy