YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 04/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

DAY 17 OF 30

Ayubu alikuwa mcha Mungu (Ayu 1:1). Wengi tumeamini kuwa tukiwa hivyo, maisha yatakuwa ya raha tupu. Lakini hapa twaona Ayubu akiteseka na kukata tamaa. Kaburi ni njia pekee anayoiona. Dhihaka za watu (m.2 BHN, Wanaonidhihaki wamenizunguka, dhihaka zao naziona dhahiri) na majonzi (m.7, Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli) vimempofusha asione tumaini tena kuhusu maisha ya raha ng'ambo ya kaburi. Mungu anatufundisha kuwa kama tukimwamini Yesu, kaburi ni njia tunayopita kuelekea pumziko la furaha na amani milele. Basi, tusione mateso ya sasa, na hata kifo kinachotukaribia, ni mwisho mbaya.

Scripture

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 04/2020

Soma Biblia Kila Siku 04/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Luka, Zaburi na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma mpango huu

More