YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 2Sample

Soma Biblia Kila Siku 2

DAY 3 OF 28

Huu ni wimbo wa Daudi wa shukrani. Mistari miwili inaeleweka vizuri zaidi kwa Kiswahili cha kisasa: Wastahili sifa, ee Mungu, huko Siyoni, watu watakutimizia wewe ahadi zao (m.1). Ulimwengu wote washangazwa na matendo yako. Wasababisha furaha kila mahali, toka mashariki hata magharibi (m.8). Daudi ana sababu tatu za kushukuru: 1. Ondoleo la dhambi na hali yake ya kuwa karibu na Mungu (m.1-4). 2. Uweza wa Mungu unaoonekana duniani kote (m.5-8). 3. Baraka yake ya kuleta ustawi sana katika nchi (m.9-13). Tusisahau shukrani!