YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 2Sample

Soma Biblia Kila Siku 2

DAY 2 OF 28

Lawi alikuwa ameshakufa tangu muda mrefu. Kwa hiyo "mtu mmoja wa nyumba ya Lawi" na "binti mmoja wa Lawi", wote wawili ni kutoka ukoo wa Lawi, si watoto wake. Ingawa Waisraeli walikuwa wanateseka, shetani hakuweza kuvunja mpango wa Mungu wa kuwaokoa wana wa Israeli kwa mkono wa Musa. Kwa hiyo shetani alishindwa kumwua Musa kwa mkono wa Wamisri. Hata maadui wa Mungu wamebidi wamtii Mungu na mpango wake, kama kwa mfano binti Farao aliyemwokoa Musa, na Herode ambaye mpango wake wa kumwua Yesu ulishindikana. Soma Warumi 8:31-39.

Scripture