YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 2Sample

Soma Biblia Kila Siku 2

DAY 6 OF 28

Wakati wa Agano la Kale Mwana wa Mungu alijidhihirisha kama "malaika wa Bwana". Linganisha m.2a na m.4. Maana yake ni kwamba Musa alimwona Kristo, Bwana wetu, kijitini (m.6). Wakati wa Agano la Kale palikuwapo mahali maalumu patakatifu ambapo mtu aliweza kumkaribia Mungu. Sharti lilikuwa kwamba afanye maandalizi maalum asije kufa. Lakini baada ya Kristo kufanyika mwili, kuteswa, kufa na kufufuka si hivyo tena. Sasa twaweza kumwabudu Mungu mahali popote kwa sababu ya ukombozi wa Yesu! Soma Yohana 4:20-24 na Waebrania 10:19-22.

Scripture