YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 1Sample

Soma Biblia Kila Siku 1

DAY 4 OF 31

Watu walimwona Yohana kuwa mtu mkubwa, lakini hakujivuna. Uaminifu na unyenyevu wa Yohana ulitokana na yeye kujawa na kumtukuza Yesu. Akijihesabu kuwa hastahili hata kuwa mtumwa wa Yesu (m.27), aliona heshima yake mwenyewe ni kumshuhudia Yesu kwa watu wote. Alimtambulisha kuwa ndiye Kristo aliyetumwa na Mungu kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu. Hakika ndivyo alivyo Bwana Yesu. Alizichukua dhambi zote za ulimwengu. Tukimtazama yeye hata kumwamini, tunao uzima wa milele.

Scripture