YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 1Sample

Soma Biblia Kila Siku 1

DAY 7 OF 31

Ilibakia kidogo Bwana arusi wa Kana kufedheheka kwa kuwa alitindikiwa kinywaji kwa ajili ya wageni wa sherehe. Aliokoka kutoka fedheha hii kwa sababu: Mosi, alimwalika Bwana Yesu katika arusi yake, na pili, alisikia na kuamini neno aliloambiwa naye. Je, na wewe unafanya sherehe kwa namna ileile? Na ikiwa umeoa au kuolewa, je, Yesu ni Bwana vilevile katika ndoa yako? Kama jibu lako ni ”ndiyo”, hata sherehe au ndoa yakoitakuwa ishara inayodhihirisha utukufu wa Yesu kama ilivyotokea kule Kana!

Scripture