Faraja Ya Majaliwa Ya Munguគំរូ

Faraja Ya Majaliwa Ya Mungu

ថ្ងៃទី 3 ក្នុងចំណោម 3 ថ្ងៃ

Kuendelea kutoka jana, ikiwa ufalme wa Mungu unaweza kufahamika kwa kina, ndivyo ilivyo ajenda ya ufalme wake. Ajenda ya ufalme, basi, inaweza kufafanuliwa kama udhihirisho unaoonekana wa utawala kamili wa Mungu juu ya kila eneo la maisha. Hilo lina hatari kubwa kwetu. Sababu ya wengi wetu waamini kuhangaika ni kwamba tunataka Mungu abariki ajenda yetu badala ya sisi kutimiza yake. Tunataka Mungu aimarishe mipango yetu badala ya kutimiza yake. Tunataka Mungu atuletee utukufu kuliko sisi kumletea utukufu.

Lakini haifanyi kazi kwa njia hiyo. Mungu ana mpango mmoja tu: Mpango wake wa ufalme. Tunahitaji kujua hiyo ni nini ili tuweze kuhakikisha kuwa tunafanya kazi katika mpango wa Mungu, sio wetu.

Neno la Kigiriki ambalo Biblia hutumia kumaanisha ufalme ni basileia, ambalo kimsingi linamaanisha “utawala” au “mamlaka.” Imejumuishwa katika ufafanuzi huu ni dhana ya uwezo. Kwa hivyo tunapozungumza juu ya ufalme, tunazungumza kwanza juu ya mfalme au mtawala. Tunazungumza juu ya mtu anayesimamia. Sasa ikiwa kuna mtawala, lazima pia kuwe na “watawaliwa,” au raia wa ufalme. Aidha, ufalme unajumuisha eneo; yaani, eneo ambalo mfalme anatawala. Iwapo utakuwa na mtawala, sheria na eneo, unahitaji pia kanuni za ufalme, mwongozo unaoongoza uhusiano kati ya mtawala na raia. Hizi ni muhimu ili watawaliwa wajue wapo wanafanya kile ambacho mtawala anataka kifanywe. Hatimaye, pia kuna waasi. Sisi sote tunaanza kuasi dhidi ya utawala wake Mungu; Inamchukua kazi ya kulainisha mioyo yetu na kutubadilisha kutoka katika hali ya uasi na kutufanya tuwe watawaliwa.

Ufalme wa Mungu unajumuisha vipengele hivi vyote. Yeye ndiye Mtawala kamili wa milki yake, ambayo inajumuisha viumbe vyote. Vivyo hivyo, mamlaka Yake ni jumla. Kila kitu Mungu anatawala, Yeye anakiendesha — hata wakati hakionekani kama anakiendesha. Hata wakati maisha yanaonekana kama hayawezi kudhibitiwa, Mungu anaendesha katika hali hiyo ionekanayo kana kwamba inje ya udhibiti.

Unaweza kujisikia peke yako, lakini hauko peke yako.

Unaweza kujihisi kuwa umesahaulika, lakini haujasahaulika.

Mungu anatawala juu ya yote na katika yote. Anakutafutia mema yako makuu anapouendeleza ufalme wake duniani, kwa utukufu wake.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

អំពី​គម្រោងអាន​នេះ

Faraja Ya Majaliwa Ya Mungu

Maisha yana namna ya kukufanya ujisikie kana kwamba umesahaulika. Iwe ni wakati maisha yanapoanza kugeuka kuwa mabaya au wakati mambo yanaonekana hayaendi sawa, Mungu ana mpango na wewe. Katika mpango huu wa siku 3, Tony Evans anafundisha jinsi Mungu anavyodhibiti kila kitu, haijalishi kinaonekana kibaya kiasi gani.

More