Zaburi 54
54
Maombi ya kujikinga na waadui
1-2Kwa mukubwa wa waimbaji: kwa vyombo vyenye nyuzi. Mashairi ya Daudi, yanayoelekea wakati mutu mumoja kutoka Zifu alipomwendea Saulo na kumujulisha kwamba Daudi amejificha kwao.
3Ee Mungu,
uniokoe kwa jina lako,
unitetee kwa nguvu zako.
4Ee Mungu, usikilize maombi yangu;
uyategee sikio maneno ya kinywa changu.
5Watu wenye kiburi wananishambulia,
watu wakali wanawinda maisha yangu,
watu ambao hawamujali Mungu.
6Ninajua Mungu ni musaada wangu,
Yawe anaimarisha maisha yangu.
7Yeye atawaazibu waadui zangu kwa uovu wao wenyewe;
kwa uaminifu wako, ee Mungu, uwaangamize.
8Nitakutolea sadaka kwa moyo wa furaha;
nitalisifu jina lako maana wewe ni muzuri.
9Umeniokoa katika taabu zangu zote,
nami nimewaona waadui zangu wameshindwa.
Currently Selected:
Zaburi 54: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.