YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 3

3
Kuomba musaada
Furaha ya kweli
1Zaburi ya Daudi. Inaelekea wakati alipomukimbia mwana wake Abusaloma.
2Ee Yawe,
angalia ginsi waadui zangu wanavyokuwa wengi.
Ni wengi sana hao wanaonishambulia.
3Wengi wanasema juu yangu:
“Hautapata musaada wowote kwa Mungu.”
4Lakini wewe, ee Yawe, unanizunguka kama ngao;
kwako ninapata utukufu na ushindi.
5Ninakulilia kwa sauti, ee Mungu,
nawe unanisikiliza kutoka kwenye mulima wako mutakatifu.
6Ninalala na kupata usingizi,
ninaamuka tena, maana wewe ni tegemeo langu.
7Sitaogopa maelfu ya watu
wanaonizunguka kila upande.
8Ee Yawe,
ee Mungu wangu,
wewe unayevunja waadui zangu wote mataya,
unayeponda waovu meno,
simama sasa uniokoe!
9Yawe ndiwe unayeokoa;
uwape baraka watu wako.

Currently Selected:

Zaburi 3: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in