YouVersion Logo
Search Icon

1 Wathesalonike 2

2
Huduma ya Paulo katika Thesalonike
1 # 1 The 1:5,9; 2 The 3:7 Maana ninyi wenyewe, ndugu, mnakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure; 2#Mdo 16:19-24; 17:1-9 ingawa tuliteswa na kutukanwa, katika Filipi kama mjuavyo, tulithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana. 3Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila; 4#Yer 11:20; Gal 1:10; 1 Tim 1:11 bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu. 5#Mdo 20:33; Mk 12:40; 2 Pet 2:3 Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wowote, kama mjuavyo, wala maneno ya juu juu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi. 6#Yn 5:41,44 Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine, ingawa tungeweza kuwalemea kama Mitume wa Kristo; 7bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. 8Hivyo ndivyo nasi tukiwajali kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu. 9#1 Kor 4:12; Mdo 20:34 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, huku tukiwahubiria Injili ya Mungu. 10Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa; 11#Mdo 20:31 vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia; 12#Efe 4:1; Flp 1:27; 2 The 1:5; 1 Pet 5:10 ili mwende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.
13 # 1 The 1:2; Gal 1:11; 2 The 2:13 Kwa sababu hiyo sisi nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe wa Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na kwa kweli ndivyo lilivyo; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini. 14#Mdo 17:5 Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yudea, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi; 15#Mdo 2:23; 7:52; 9:23,29; 13:45,50; 14:2,5,19; 17:5,13; 18:12 ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wowote; 16#Mwa 15:16; Mt 23:32,33 huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho.
Hamu ya Paulo ya kuwatembelea Wathesalonike tena
17 # Rum 1:11,13 Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa muda, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu. 18Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, nilitaka kuja mara kwa mara, lakini Shetani akatuzuia. 19#Flp 2:16; 4:1; 2 The 1:4 Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji la kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake? 20Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha yetu.

Currently Selected:

1 Wathesalonike 2: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy