YouVersion Logo
Search Icon

1 Wathesalonike 1

1
Salamu
1 # Mdo 17:1; 15:40; 2 The 1:1 Paulo, Silwano na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.
Imani na kielelezo cha Wathesalonike
2 # 2 The 1:11 Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu. 3#1 Kor 13:13; Kol 1:4,5 Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na subira yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu. 4Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, tunajua uteule wenu; 5#1 Kor 2:5 ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu. 6#Mdo 17:5-9; 13:52; 1 Kor 4:16; 2 The 3:9 Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu. 7#1 The 4:10; Flp 3:7; 1 Pet 5:3 Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.
8 # Rum 1:8 Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lolote. 9#Mdo 14:15; Yn 17:3; 1 Kor 12:2 Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli; 10#1 The 5:9; Tit 2:13; Mdo 17:31 na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa kutoka kwa ghadhabu itakayokuja.

Currently Selected:

1 Wathesalonike 1: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy