YouVersion Logo
Search Icon

1 Wathesalonike 3

3
1 # Mdo 17:14,15 Basi kwa hiyo, tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tuliona vema kuachwa Athene peke yetu. 2#Mdo 16:1-3 Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji katika imani yenu; 3#Efe 3:13; 2 Tim 3:12; 2 The 1:4 mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa ndizo tulizowekewa. 4#2 The 3:10; Mdo 14:22 Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mnajua. 5#Flp 2:16 Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
Ripoti ya Timotheo ya kutia moyo
6 # Mdo 18:5 Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea Habari Njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona kama vile nasi tunavyotamani kuwaona ninyi. 7#2 The 1:4 Kwa sababu hiyo, ndugu, katika dhiki na mateso yetu yote, katika habari zenu, tumefarijiwa kwa imani yenu. 8Kwa kuwa sasa tunaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana. 9Maana ni shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu; 10usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu, na kuurekebisha upungufu wa imani yenu?
11 # 2 The 2:16 Basi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze njia yetu tufike kwenu. 12Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; 13#Flp 1:10; 2 The 1:7,10 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

Currently Selected:

1 Wathesalonike 3: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy