YouVersion Logo
Search Icon

Zab 89

89
Agano la Mungu wa Daudi
Utenzi wa Ethani Mwezrahi.
1Fadhili za BWANA nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
2Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.
3 # Eze 34:23; Hes 3:5; Mdo 2:30; Ebr 7:21 Nimefanya agano na mteule wangu,
Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.
4 # 2 Sam 7:12-16; 1 Fal 9:5; 1 Nya 17:11-14; Zab 132:11; Isa 9:6,7; Lk 1:32; Mdo 2:30; Rum 1:3 Wazao wako nitawafanya imara milele,
Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.
5Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako,
Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.
6Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA?
Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika?
7Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu,
Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
8BWANA, Mungu wa majeshi,
Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU?
Na uaminifu wako unakuzunguka.
9 # Ayu 38:11; Nah 1:4; Mt 8:26 Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari.
Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.
10 # Isa 30:7 Ndiwe uliyemseta Rahabu akawa kama aliyeuawa,
Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao.
11Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako,
Ulimwengu na vyote viujazavyo
Ndiwe uliyeupiga msingi wake.
12 # Yos 19:22; 12:1; Amu 4:6 Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba,
Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13Mkono wako ni mkono wenye uweza,
Mkono wako una nguvu,
Mkono wako wa kuume umetukuka.
14Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako,
Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.
15 # Hes 10:10 Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,
Ee BWANA, huenenda katika nuru ya uso wako.
16Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,
Na kwa haki yako hutukuzwa.
17Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe,
Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.
18 # Hos 13:10 Maana ngao yetu ina BWANA,
Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.
19Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi,
Ukasema, nimempa aliye hodari msaada;
Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
20 # 1 Sam 13:14; 16:12; Mdo 13:22 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,
Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
21Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake,
Na mkono wangu utamtia nguvu.
22Adui hatamwonea,
Wala mwana wa uovu hatamtesa.
23Bali nitawaponda watesi wake mbele yake,
Nitawapiga wanaomchukia.
24 # Zab 61:7 Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo,
Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.
25Nitaweka mkono wake juu ya bahari,
Na mkono wake wa kuume juu ya mito.
26 # 2 Sam 7:14; 1 Nya 22:10; Yn 5:17 Yeye ataniita, Wewe baba yangu,
Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
27 # Zab 2:7; Ufu 1:5 Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza,
Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.
28Hata milele nitamwekea fadhili zangu,
Na agano langu litafanyika amini kwake.
29 # Isa 9:7; Yer 33:17; Dan 7:14; Kum 11:21 Wazao wake nao nitawadumisha milele,
Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.
30 # 2 Sam 7:14; Yer 9:13 Wanawe wakiiacha sheria yangu,
Wasiende katika hukumu zangu,
31Wakizihalifu amri zangu,
Wasiyashike maagizo yangu,
32Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo,
Na uovu wao kwa mapigo.
33Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye,
Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.
34Mimi sitalihalifu agano langu,
Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu.
35 # Zab 110:4; Ebr 6:13,17; Amo 4:2; 8:7 Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu,
Hakika sitamwambia Daudi uongo,
36 # 2 Sam 7:16; Lk 1:33; Yn 12:34 Wazao wake watadumu milele,
Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu.
37 # Yer 31:35 Kitathibitika milele kama mwezi;
Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.
38Walakini Wewe umemtupa na kumkataa,
Umemghadhibikia masihi#89:38 Au, mtiwa mafuta. wako.
39 # Omb 5:16 Umechukizwa na agano la mtumishi wako,
Umeinajisi taji yake na kuitupa chini.
40Umeyabomoa maboma yake yote,
Umezifanya ngome zake kuwa magofu.
41Wote wapitao njiani wanateka mali zake;
Amekuwa laumu kwa jirani zake;
42Umeutukuza mkono wa kuume wa watesi wake;
Umewafurahisha wote wanaomchukia.
43Pia umeurudisha nyuma ukali wa upanga wake;
Wala hukumsimamisha vitani.
44Umeikomesha fahari yake;
Kiti chake cha enzi umekitupa chini.
45Umezipunguza siku za ujana wake;
Umemvika aibu.
46Ee BWANA, hata lini? Utajificha hata milele?
Ghadhabu yako itawaka kama moto?
47 # Ayu 7:7 Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu;
Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!
48 # Ebr 11:5 Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti,
Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?
49 # 2 Sam 7:15; Isa 55:3 Bwana, zi wapi fadhili zako za kwanza,
Ulizomwapia Daudi kwa uaminifu wako?
50Ee Bwana, ukumbuke,
Wanavyosimangwa watumishi wako;
Jinsi ninavyostahimili kifuani mwangu
Masimango ya watu wengi.
51Ambayo adui zako wamesimanga, Ee BWANA,
Naam, wamezisimanga hatua za masihi#89:51 Au, mtiwa mafuta. wako.
* * *
52Na ahimidiwe BWANA milele. Amina na Amina.

Currently Selected:

Zab 89: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy