YouVersion Logo
Search Icon

Zab 88

88
Sala ya Msaada katika Wakati wa Kukata Tamaa
Wimbo. Zaburi ya Wakorahi. Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi.
1Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu
Mchana na usiku nimelia mbele zako.
2Maombi yangu yafike mbele zako,
Uutegee ukelele wangu sikio lako.
3Maana nafsi yangu imeshiba taabu,
Na uhai wangu umekaribia kuzimu.
4Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni;
Nimekuwa kama mtu asiye na msaada.
5Miongoni mwao waliokufa nimetupwa,
Kama waliouawa walalao makaburini.
Hao ambao Wewe huwakumbuki tena,
Wametengwa mbali na mkono wako.
6Mimi umenilaza katika shimo la chini,
Katika mahali penye giza vilindini.
7Ghadhabu yako imenilemea,
Umenitesa kwa mawimbi yako yote.
8Wanijuao umewatenga nami;
Umenifanya kuwa chukizo kwao;
Nimefungwa wala siwezi kutoka.
9Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso
BWANA, nimekuita kila siku;
Nimekunyoshea Wewe mikono yangu.
10Wafu je! Utawafanyia miujiza?
Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?
11Fadhili zako zitasimuliwa kaburini?
Au uaminifu wako katika uharibifu?
12 # Ayu 10:21; Zab 31:12; Mhu 8:10 Miujiza yako itajulikana gizani?
Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?
13Lakini mimi nimekulilia Wewe, BWANA,
Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.
14BWANA, kwa nini kuitupa nafsi yangu,
Na kunificha uso wako?
15 # Ayu 6:4; Isa 53:8; Dan 9:26 Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana,
Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.
16Hasira zako kali zimepita juu yangu,
Maogofyo yako yameniangamiza.
17Yamenizunguka kama maji mchana kutwa,
Yamenisonga yote pamoja.
18 # Ayu 19:13 Mpenzi na rafiki umewatenga nami,
Nao wanijuao wamo gizani.

Currently Selected:

Zab 88: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy