YouVersion Logo
Search Icon

Zab 90

90
KITABU CHA NNE
Mungu Adumuye Milele na Binadamu Apitaye
Sala ya Musa, Mtu wa Mungu.
1Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu,
Kizazi baada ya kizazi.
2 # Ayu 38:4-6; Mit 8:25 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3 # Mwa 3:19; Mhu 12:7 Wamrudisha mtu mavumbini,
usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4 # Ebr 13:8; 2 Pet 3:8 Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
5 # Isa 40:6 Wawagharikisha, huwa kama usingizi,
Asubuhi huwa kama majani yameayo.
6 # Ayu 14:2; Zab 92:7 Asubuhi yachipuka na kumea,
Jioni yakatika na kukauka.
7Maana tumetoweshwa kwa hasira yako,
Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.
8 # Zab 50:21; Yer 16:17; Zab 19:12; Mit 5:21; Mhu 12:14; Rum 2:16; 1 Kor 4:5; Ebr 4:12,13 Umeyaweka maovu yetu mbele zako,
Siri zetu katika mwanga wa uso wako.
9Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako,
Tumetowesha miaka yetu kama kite.
10Siku za miaka yetu ni miaka sabini,
Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;
Na kiburi chake ni taabu na ubatili,
Maana chapita upesi tukatokomea mara.
11Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako?
Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?
12 # Zab 39:4 Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
13 # Kum 32:36 Ee BWANA urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako.
14Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
15Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa,
Kama miaka ile tuliyoona mabaya.
16 # Zab 44:1; Hab 3:2 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,
Na adhama yako kwa watoto wao.
17 # Isa 26:12; 2 The 2:16,17 Na uzuri wa BWANA, Mungu wetu, uwe juu yetu,
Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti,
Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.

Currently Selected:

Zab 90: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy