YouVersion Logo
Search Icon

Kum 6

6
Amri Kuu
1Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; 2#Kut 20:2-20; Zab 111:10; 128:1; Mhu 12:13; Mit 3:1upate kumcha BWANA, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. 3Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali.
4 # Mk 12:29; Isa 9:6; Yn 1:1; 10:30; 17:3; 1 Kor 8:4; Efe 4:6; Flp 2:5,6 Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. 5#Mt 22:37; Mk 12:30-32; Lk 10:27; Kum 30:6; 1 Yoh 5:3Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6#Kum 11:18-20; Isa 51:7Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7#Efe 6:4nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8#Mit 6:21; Kut 13:9; Mit 3:3; 7:3Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9#Kum 11:20; Isa 50:8; 57:8Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
Hadhari ya Kutotii
10 # Mwa 12:7; 26:3; 28:13; Yos 24:13; Zab 105:44 Tena itakuwa atakapokwisha BWANA, Mungu wako, kukuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe, 11na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vimefukuliwa usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba; 12ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa. 13#Mt 4:10; Lk 4:8; Kum 13:4; Zab 63:11Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake. 14#Yer 25:6Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao; 15kwani BWANA, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya BWANA, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi.
16 # Kut 17:1-7; Mt 4:7; Lk 4:12; 1 Kor 10:9 Msimjaribu BWANA, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa. 17#Zab 119:4Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza. 18Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa BWANA; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri BWANA aliyowaapia baba zako, 19ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, kama alivyosema BWANA.
20Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N’nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu? 21Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu; 22BWANA akaonya ishara na maajabu, makubwa, mazito, juu ya Misri, na juu ya Farao, na juu ya nyumba yake yote, mbele ya macho yetu; 23akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia baba zetu. 24#Ayu 35:7,8; Yer 32:39; Zab 41:2; Lk 10:28BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo. 25#Rum 10:3Tena itakuwa haki kwetu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.

Currently Selected:

Kum 6: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy