YouVersion Logo
Search Icon

Kum 7

7
Watu Wateule wa Bwana
1 # Mdo 13:19 BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang’oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 2#Yos 6:17; 11:11; Kut 23:32; Yos 2:14; Amu 1:24; 2:2wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; 3#Yos 23:12; 1 Fal 11:2; Ezr 9:2binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. 4Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi. 5#Kum 12:3; Kut 23:24; 34:13Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.
6 # Kut 19:5; Kum 4:20; 14:2; 26:18; Tit 2:14; 1 Pet 2:9; Zab 50:5; Yer 2:3; Amo 3:2; 1 Kor 6:19,20; Zab 135:4 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi. 7BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; 8#Kut 32:13; Zab 105:8; Lk 1:55; Kut 13:3bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. 9#Kut 20:5-6; 34:6-7; Hes 14:18; Kum 5:9-10; Isa 49:7; 1 Kor 1:9; 10:13; 2 Kor 1:18; 1 The 5:24; 2 Tim 2:13; Ebr 11:11; 1 Yoh 1:9; Neh 1:5; Dan 9:4Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; 10#Zab 21:8; Mit 11:31; Isa 59:18; Nah 1:2; Rum 12:19naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake. 11Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazokuamuru leo, uzitende.
Baraka za Utiifu
12 # Kum 11:13-17 Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako; 13#Kut 23:25; Zab 1:3; 11:7; Mit 15:9; Yn 14:21; 1 Yoh 2:5naye atakupenda na kukubarikia na kukuongeza tena ataubarikia uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, maongeo ya ng’ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa. 14Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo. 15#Kut 9:14; 15:26; Kum 28:27; Zab 105:37Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao. 16#Amu 8:27; Zab 106:36Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo. 17#Hes 33:53Nawe kama ukisema moyoni mwako, Mataifa haya ni mengi kunipita mimi; nitawatoaje katika milki yao? 18#Amu 6:13; Zab 77:11; 105:5; 135:8-10; Isa 63:11-15Usiwaogope; kumbuka sana BWANA, Mungu wako, alivyomfanya Farao na Misri yote; 19uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje BWANA, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya BWANA, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa. 20#Kut 23:28; Yos 24:12Tena BWANA, Mungu wako, atampeleka mavu kati yao, hata hao watakaosalia, hao wajifichao, waangamie mbele zako. 21#Hes 14:9; 16:3; Yos 3:10; Kum 10:17; Neh 1:5; 4:14; 9:32Usiingiwe na kicho kwa sababu yao; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu katikati yako, Mungu mkuu, mwenye utisho. 22Naye BWANA, Mungu wako, atayatupia nje mataifa yale mbele yako kidogo kidogo; haikupasi kuwaangamiza kwa mara moja, wasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu. 23Ila BWANA, Mungu wako, atawatoa mbele yako, atawatia mashaka, mashaka makuu, hata waishe kuangamizwa. 24#Yos 10:24; 12:1; Kum 11:25; Yos 1:5; 10:8; 23:9Na wafalme wao atakutilia mkononi mwako, nawe utalipoteza jina lao litoke chini ya mbingu; hapana mtu atakayeweza kusimama mbele yako, hata utakapokwisha kuwaangamiza. 25#Kut 32:20; Kum 12:3; 1 Nya 14:12; Kut 20:17; Yos 7:1; Lk 12:15; Kol 3:5; Amu 8:27; Sef 1:3; Kum 17:1Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako; 26#Law 27:28; Yos 6:17na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa.

Currently Selected:

Kum 7: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy