YouVersion Logo
Search Icon

Kum 5

5
Amri Kumi
1Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia kuzitenda. 2#Kut 19:5; 24:7,8; Kum 4:23; Ebr 8:6-13; 9:19-23BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu. 3#Mt 13:17; Ebr 8:9BWANA hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai. 4#Kut 19:9,19; 20:22; Kum 4:33,36; 34:10BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto; 5#Kut 19:16; 20:21; Hes 16:48; Zab 106:23; Yer 30:21; Gal 3:19; Ebr 12:18,19; Kut 24:2(nami wakati ule nalisimama kati ya BWANA na ninyi, ili kuwaonyesha neno la BWANA; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema,
6 # Kut 20:2; Law 26:1; Kum 6:4; Zab 81:10 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
7 # Kut 20:3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
8 # Law 26:1; Kum 4:15-18; 27:15; Kut 20:4; Zab 97:7; Mdo 17:29 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. 9#Kut 34:6-7; Hes 14:18; Kum 7:9-10Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10#Yer 32:18; Dan 9:4; 1 Yoh 1:7nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
11 # Law 19:12; Kut 20:7; Yak 5:12; Mt 5:33 Usilitaje bure Jina la BWANA, Mungu wako; maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.
12 # Kut 16:23-30; 31:12-14; Kut 20:8; Neh 13:31 Ishike siku ya Sabato uitakase, kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru. 13#Kut 23:12; 31:15; 34:21; 35:2; Law 23:3; Eze 20:12Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 14#Mwa 2:2; Kut 16:29; Ebr 4:4lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe. 15Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
16 # Kum 27:16; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2,3; Law 19:3; Kol 3:20; Kum 4:40 Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
17 # Mwa 9:6; Law 24:17; Mt 5:21; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11 Usiue.
18 # Law 20:10; Mt 5:27; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11 Wala usizini.
19 # Law 19:11; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9 Wala usiibe.
20 # Kut 23:1; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; 1 Fal 21:10 Wala usimshuhudie jirani yako uongo.
21 # Rum 7:7; 13:9; Mik 2:2; Hab 2:9; Lk 12:15; Gal 5:14 Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako.
Musa Mwakilishi wa Mapenzi ya Mungu
22 # Ebr 12:18-19; Kut 24:12 Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa. 23Ikawa, mlipoisikia sauti ile toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa kabila zenu, na wazee wenu, 24mkasema, Tazama, BWANA, Mungu wetu, ametuonyesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi. 25Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya BWANA, Mungu wetu, tutakufa. 26#Kum 4:33Maana katika wote wenye mwili ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife? 27#Ebr 12:19Enenda karibu wewe, ukasikie yote atakayoyasema BWANA, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia BWANA, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda. 28Naye BWANA akasikia sauti ya maneno yenu mliyoniambia; BWANA akaniambia, Nimesikia sauti ya maneno ya watu hawa waliyokuambia; wamesema vema yote waliyosema. 29#Kum 32:29; Zab 81:13; Isa 48:18; Yer 44:4; Mt 23:37; Lk 19:42; 2 Kor 5:20; 6:1; 7:1; Ebr 12:25; Kum 11:1; Zab 119:1-5; Lk 11:28; Yn 15:14; Ufu 22:14Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele! 30Enda uwaambie, Rudini hemani mwenu. 31#Mal 4:4; Gal 3:19Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitanena nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki. 32#Kum 17:20; 28:14; Yos 1:7; 23:6; Mit 4:27Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kuume wala wa kushoto. 33#Kum 10:12; Zab 119:6; Mhu 8:12; Yer 7:23; Lk 1:6; 1 Tim 4:8; Kum 4:40; 12:25,28; 22:7; Efe 6:3Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.

Currently Selected:

Kum 5: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy