1
Isaya 54:17
BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
SWC02
Silaha zote zilizotengenezwa kwa kukuzuru wewe hazitafaa kwa kitu chochote. Mutu akikushitaki, utamushinda. Hiyo ndiyo haki niliyowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowahakikishia. –Ni ujumbe wa Yawe.
Compare
Explore Isaya 54:17
2
Isaya 54:10
Milima inaweza kutoweka, vilima vinaweza kuondolewa, lakini rehema zangu kwako sitaziacha, agano langu la amani litaimarishwa. Ni Yawe anayekuhurumia anayesema hivyo.
Explore Isaya 54:10
3
Isaya 54:4
Usiogope, hautapata haya tena. Usifazaike, hautazarauliwa tena. Utaisahau haya uliyopata katika ujana wako, wala hautakumbuka tena mazarau ya ujane wako.
Explore Isaya 54:4
4
Isaya 54:5
Muumba wako atakuwa mume wako. Jina lake Yawe wa majeshi. Mukombozi wako ni Mutakatifu wa Israeli. Yeye anaitwa Mungu wa Ulimwengu Wote.
Explore Isaya 54:5
5
Isaya 54:2
Panua nafasi katika hema yako, ongeza mapazia ya makao yako, usijali mali unayotumia. Urefushe kamba zako, na kuimarisha misumari yako
Explore Isaya 54:2
6
Isaya 54:13
Watu wako watafundishwa nami Yawe, wana wako watapata ustawi mwingi.
Explore Isaya 54:13
7
Isaya 54:8
Kwa hasira nyingi nilikuficha uso wangu kwa muda kidogo, lakini kwa wema wa milele nitakuonea huruma. Ni Yawe Mukombozi wako anayesema hivyo.
Explore Isaya 54:8
8
Isaya 54:7
Nilikuacha kwa muda mufupi tu. Kwa huruma nyingi, nitakurudisha.
Explore Isaya 54:7
9
Isaya 54:9
Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa. Wakati ule niliapa kwamba sitaifunika tena dunia kwa mafuriko ya maji. Basi sasa ninaapa kwamba sitakukasirikia tena wala sitakukaripia tena.
Explore Isaya 54:9
10
Isaya 54:12
Minara yako nitaijenga kwa mawe ya akiki, milango yako kwa almasi, na ukuta wako kwa mawe ya bei kali.
Explore Isaya 54:12