Basi, nikatoa unabii kama nilivyoamriwa. Nilipokuwa nikitoa unabii, kukatokea kelele kama ya mukwaruzo na ile mifupa ikaanza kusogeleana na kuungana. Niliangalia, nikaona ile mifupa imewekewa mishipa na nyama na kufunikwa kwa ngozi. Lakini haikukuwa na uzima.