Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Maarifa ya Mungu ni ya ajabu. Mtu hawezi kuyafikia. Ingawa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hatuna maarifa na hekima ya kujua kilichoumbwa na Mungu. Tunajisifu kwa sababu ya maendeleo na ujuzi uletwao na sayansi na teknolojia yake. Lakini Mungu ana swali kwa Ayubu na sisi wa kizazi cha leo: Maendeleo hayo yana faida gani katika maisha ya kumwamini Mungu? Mazungumzo ya Mungu na Ayubu yatusogeze mbele kwenye hatua ya kumfahamu Mungu zaidi. (Ukiwa na Tenzi za Rohoni, imba au omba na. 92.)