Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Majibu ya Mungu kwa Ayubu yanakusudia kumfundisha kuwa Mungu ni Mwenyezi, hapimiki. Uwezo na ujuzi wa mtu uko chini ya Mungu. Changamoto alizo nazo Ayubu hazizidi wala hazifai kuwekwa katika kapu moja na uweza wa Mungu. Maswali anayoulizwa Ayubu yanathibitisha mwanadamu alivyo na uwezo mdogo juu ya Mungu. Mungu hahitaji majibu. Huu sio mtihani wa kujibiwa bali ni kuvuta unyenyekevu wa mtu kwa Muumba wake. Ndivyo anavyokusudia Mungu akituhoji. Mbele ya Mungu mtu anajipambanua alivyo.