Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Mbele ya ukuu wa Mungu mwanadamu ni sehemu ya uumbaji. Mtu asipotafakari kazi ya Mungu kwa unyenyekevu, anajifanya mjinga. Kiburi chake huzuia asione nuru itokayo kwa utukufu wa Mungu. Unyeyekevu sio udhaifu, bali ni kukubali makuu ya Mungu. Ni kuwa tayari kuongozwa na Mungu kwenye nuru yake. Tukubali ujinga wetu kama tupo pasipo nuru hiyo. Hatujui lini tutakufa, wakati wa vita wala mafuriko. Tujiweke mikononi mwa Mungu ili atupe hekima na kutujulisha yaliyo mapenzi yake yenye heri.