Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Elihu anaendelea kumweleza Ayubu kuhusu ukuu wa Mungu. Mungu hawezi kumdharau mtu yeyote, maana ni Muumba wetu; na uhodari wake hauwezi kushindwa anapotafuta kumponya aliyetaabika. Kutokusikia maonyo ya Mungu huleta maangamizi. Lakini tukizingatia ukuu wake na kujitambua kama viumbe vyake, tunasaidiwa kuwa na unyenyekevu wala si madai, hata tunaposhindwa kuelewa taabu yetu. Tunaanza kugundua kuwa Mungu humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake (m.15). Zingatia maneno haya “kwa njia ya”! Hutuvuta kulilia msaada wa Mungu.