Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Anayosema Elihu, je, ni maswali ya kumdharau Ayubu? Siyo kwamba Ayubu ameshajua hayo yote na kumwamini Mungu? Ndiyo. Hata hivyo tunahitaji kukumbushwa ukuu utishao wa Mungu ili tusifanane na wale walio na hekima mioyoni (m.24). Ni watu wanaotafuta hekima kwao wenyewe badala ya kuzifikiri kazi za Mungu za ajabu. Tufanye anavyoshauri Elihu katika m.14: Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. Sisi binadamu tunalo giza fulani katika kumfahamu Mwenyezi. Hatuwezi kumwona. Ndiyo maana mwishoni Elihu anakiri kuwa tunapaswa kunyenyekea mbele ya Mungu wakati wote.