Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Mungu anamzidishia Ayubu maarifa kumhusu yeye. Lengo ni kumwezesha ajue kuwa maswali na changamoto za maisha hazitatuliwi au kujibiwa zote na hekima au ujuzi wa binadamu. Tunachokifahamu ni kile ambacho Mungu ametujalia kutufunulia. Kufahamu hivyo, kunafungua fursa ya kumwamini Mungu: Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; nawe utanijulisha hekima kwa siri (Zab 51:6). Ujuzi anaoupokea Ayubu ni ufahamu mpya na kuongeza fursa ya kumwamini Mungu atakavyo. Siri ya Mungu i katika Neno lake.