Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

30天中的第26天

Wakati wale wazee watatu walipoongea na Ayubu, aliendelea kujitetea. Lakini tangu Elihu alipoanza kunena, Ayubu amenyamaza tu. Hivyo kuna nafasi kwa Mungu kumjibu Ayubu kwa njia ya kuthibitisha uwezo wake. Anatumia uwezo katika uumbaji ili kumwonesha Ayubu ukuu wake. Anajitambulisha mwenyewe kwa njia ya upepo wa kisulisuli. Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli (m.1), akiongea na Ayubu kama Muumbaji kwa kiumbe chake. Kama ukitaka mifano mingineyo, soma Kut 19:16-19 (ufunuo mlimani Sinai) na 1 Fal 19:11-13 (ufunuo kwa Eliya).

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More