Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Kila siku tunashuhudia mafarakano ya aina nyingi kati ya watu. Siku za leo haya mafarakano yako pia ndani ya kanisa letu. Shabaha ya Kristo ni kuleta amani kwa njia ya upatanisho kati ya Mungu na binadamu. Tukikubali kupatanishwa na Mungu, yote yanakuwa mapya: Tunasamehewa dhambi na Mungu (soma k.m. Efe 2:13-18), tunafanywa viumbe vipya mioyoni mwetu (rudia m.17), na tunapewa kusudi jipya la maisha yetu ya kuwa wajumbe wa upatanisho huo wa Mungu kuanzia pale tulipo.Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu(m.20). M.21 hujumlisha ujumbe wetu namna hii:Yeye[Mungu]asiyejua dhambi alimfanya[Yesu]kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye[Yesu].
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
