Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

SIKU 24 YA 30

Ufuasi wa Kikristo, hasa ule katika kuitangaza Injili, kunafuatana na vikwazo mbalimbali.Nje palikuwa na vita, ndani hofu, Paulo anasema. Vita hiyo ilisababishwa na maadui wa Injili, hofu yake na kutojua jinsi Wakristo walivyokuwa wanaendelea. Lakini Mungu nimwenye kuwafariji wanyonge(m.6). Tujifunze kwamba mara nyingi anatumia sisi tunaomwamini tufajiriane. Tunaweza kuwatia moyo watumishi wa Neno la Kristo kwa jinsi tunavyoishi. Tafakari Paulo anavyosema kuhusu Tito alivyokuja na kumletea taarifa juu ya Wakristo wa Korintho:Si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi(m.7). Tukumbuke pia kuwaombea ili wasikate tamaa.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana