Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

”Tokeni kati yao” wasioamini, ina maana gani kivitendo? Maneno kama 1 Kor 5:9-11 na 7:12-13 huonyesha kwamba kinacholengwa na Mtume Paulo hapa si kujitenga nao, bali kujitenga na mapatano na uasi wao na imani yao katika sanamu n.k.:Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye(1 Kor 5:9-11).Watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe(1 Kor 7:12-13).Kinachosemwa hapa ni kututaka Wakristo kutokufungamana na tabia na matendo ya wasiomwamini Kristo. Wakristo tuishi kati ya wasiomwamini Kristo kwa namna inayoonyesha kwambasisi tu hekalu la Mungu aliye hai(m.16). Soma Lk 19:1-10 ambapo Yesu mwenyewe anatoa mfano.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz